Okoa Mombasa yajiunga na KCSPOG na Natural Justice Kenya kuwasilisha maoni kuhusu Kanuni za upatikanaji wa habari

Julai 7, 2021

Okoa Mombasa, Jukwaa la Mashirika ya Kiraia ya Kenya kuhusu Mafuta na Gesi (KCSPOG) na Natural Justice Kenya wamewasilisha maoni ya pamoja kuhusu Rasimu ya Kanuni za Upatikanaji wa Taarifa (Jumla) za Kenya, 2021.

Kanuni mpya zitabainisha jinsi Mashirika ya serikali yanavyojibu maombi ya umma ya habari kupitia Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa.

Hati ya pamoja, lililowasilishwa tarehe 30 Juni 2021, ina maoni na mapendekezo ya jumla na mahususi kuzingatiwa katika uboreshaji wa Rasimu ya Kanuni. Maoni hayo yanatokana na uzoefu wa Mashirika na changamoto zinazohusiana na haki ya kupata habari, katika Nyanja mbalimbali za shughuli zao.

Ingawa kanuni zinaweza kuashiria hatua muhimu katika kuwezesha upatikanaji wa habari kwa Wakenya, maoni yanaangazia maeneo kadhaa ambapo kuna upungufu. Kwa mfano, baadhi ya maneno muhimu hayajafafanuliwa, ada za kutafsiri katika lugha za kienyeji ni nyingi kupita kiasi, hizi ni changamoto ambazo bado yanazuia ufichuzi wa taarifa muhimu.

Share This