Okoa Mombasa ya mtaka Rais Ruto kufutilia agizo kwa maandishi

Septemba 21, 2022

Okoa Mombasa leo imemtaka Rais William Ruto kugeuza mara moja – kwa maandishi – agizo la serikali linalotaka mizigo katika Bandari ya Mombasa kusafirishwa kwa kupitia Reli ya Standard Gauge (SGR).

Rais Ruto alitangaza punde tu baada ya kuapishwa kama rais wa tano wa Kenya kwamba huduma zote za bandari zitarejea Mombasa, lakini wakazi wa Mombasa bado hawajaona hatua madhubuti za kutimiza ahadi hii. Mizigo bado inalazimishwa kuingizwa kwenye SGR, na Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA), hairuhusu waagizaji wa mali kuwa na uhuru wa kuchagua vituo vya kuegeza shehena ila ya bandari ya Mombasa.

“Ahadi ya Rais Ruto ya kurudisha huduma zote za bandari Mombasa inasifiwa, lakini kufikia sasa ni maneno tu – hakuna kilichobadilika,” alisema Khelef Khalifa wa Muhuri ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalo pigania haki za kibanadamu na pia mwanachama wa Okoa Mombasa.

“Maelekezo ya shehena ya SGR yanafaa kubadilishwa kwa maandishi na KPA inahitaji kutoa mawasiliano ya maandishi ili shirika la kutoza ushuru liachilie mizigo zilizo kwa mamlaka yake. Hadi haya yote mawili yasipotelewa, hatuwezi kusema kuwa huduma za bandari zimerejea Mombasa,” Khalifa aliongeza.

Rais Uhuru Kenyatta alitoa maagizo ya shehena ya SGR mnamo 2019 ili kuunda biashara zaidi kwa SGR ambayo ilikua haingizi fedha za kutosha. Maagizo hayo yalitangazwa kwa kinyume ya sheria na Mahakama Kuu mnamo Novemba 2020, lakini serikali ilikata rufaa, kesi hiyo bado inasubiri.

Tangu 2019, maagizo hayo yameathiri uchumi wa Mombasa, ambalo inategemea sana bandari. Huku mizigo ikilazimishwa kuingia kwenye SGR, maelfu ya wamiliki wa Lori na madereva walipoteza riziki zao kwa vile hawakuhitajika tena kubeba mizigo. Mamia ya makampuni ya kusafisha na kusambaza bidhaa walihamia Nairobi au Maduka yaliyofungwa. Vituo vya shehena vya ndani vilikosa maana. Makumi ya maelfu ya watu wanaofanya kazi katika wauzaji wa malori, vituo vya huduma za mafuta, makanika, wauzaji vipuri, mikahawa, vibanda vya sekta isiyo rasmi, uchuuzi, waliachwa bila kazi.

“Kubadilisha maagizo ya shehena ya SGR ndio njia pekee ya kurejesha huduma za bandari na riziki kwa Mombasa,” Mesh Abdul Razak wa Fast Action Summit ambaye mwanachama wa Okoa Mombasa. “Hii pia ingeongeza sana ushindani wa Bandari kwa kuwapa waagizaji chaguzi zaidi za kibali cha forodha na usafiri.”

“Kurejesha huduma za bandari Mombasa hakutaharibu biashara Katika vituo vya kuweka shehena za Nairobi na Naivasha,” alisema Dennis Ombok, mshauri wa usafirishaji mali na mwanachama wa Okoa Mombasa. “Nairobi na Naivasha bado watapata mizigo. “Tunadai uhuru kwa jinsi tunavyofanya biashara. Wamiliki wa mizigo wanapaswa kuwa na uwezo wa kuchagua mambo mawili: eneo la forodha kusalimisha bidhaa zao na njia ya usafiri. Kwa sasa hawawezi kuchagua pia.”

Okoa Mombasa pia alimtaka Rais Ruto kutii agizo la mahakama ambalo halijakamilika la kuitaka serikali kutoa hadharani kandarasi na makubaliano yote yanayohusiana na mipango, ujenzi na utendakazi wa SGR. Wanachama wa Okoa Mombasa walishinda kesi hilo la agizo mahakama mwaka wa 2021, lakini serikali ya zamani ilikata rufaa.

Shilingi 450 bilioni (USD 4.2 bilioni) SGR ndio mradi wa miundomsingi ghali zaidi Katika historia ya Kenya na ulifadhiliwa Zaidi kupitia mikopo kupitia Benki ya Export-Import ya China. Kwa hayo yote bado taarifa muhimu kuhusu mradi hazijawai kuweka hadharani. Rais Kenyatta waliahidi kuweka hadharani kandarasi hizo mwaka wa 2018, lakini itashindwa kutimiza ahadi yake.

Share This