Okoa Uchumi yazindua Kushinikiza Uwajibikaji wa Madeni ya Umma Kabla ya Uchaguzi

Aprili 6, 2022

Okoa Mombasa imejiunga na muungano wa zaidi ya Mashirika 15 ya Kiraia kuzindua Kampeni ya Okoa Uchumi – mpango ambao wenye lengo kuu la kukuza uwajibikaji katika usimamizi wa deni la umma nchini Kenya.

Kampeni hiyo inasababishwa na hali mbaya ya usimamizi wa deni za Kenya, ambalo limekosa uwazi katika matumizi kulingana na sheria na mahitaji ya fedha za umma, swala ambalo limechangia kuzorota kwa uchumi na kuweka nchi kwenye mtego wa madeni. Kampeni hii imejikita katika wajibu wetu wa kuheshimu, kudumisha na kutetea Katiba ya Kenya.

Malengo manne ya kampeni ni:

  • Kuimarisha uwazi na kushiriki umma katika masuala ya deni la nchi – ikiwa ni pamoja na katika miradi kama vile Reli ya Standard Gauge (SGR)
  • Kuimarisha jukumu la usimamizi wa Bunge.
  • Kulinda uongozi na uadilifu katika usimamizi wa fedha.
  • Kulinda haki ya kutoza kodi

Tukio la uzinduzi lilijumuisha uzinduaji wa ‘Okoa Uchumi Citizen’s Manifesto for Elections 2022’ ambayo inaelezea malengo ya mpango huo na hatua mahususi zinazohitajika ili kufikia malengo hayo.tafuta fursa usome malengo hayo hapa.

Malengo hayo yanadhihirisha kua mfumo wa ushuru wa Kenya umekuwa mgumu kutokana na mahitaji makubwa ya ulipaji wa deni. Kwa sasa Kenya inatumia zaidi ya 69% ya mapato yake kulipa madeni.

Khelef Khalifa wa MUHURI ambayo ni moja wapo wa mwanachama wa Okoa Mombasa – alizungumza katika hafla ya uzinduzi, pamoja na Wanjiru Gikonyo, Dkt. Willy Mutunga, Davis Molombe, na wengineo.

Share This